Back to top

Watanzania wahimizwa kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na Corona.

21 July 2021
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari zinazotolewa na Wizara ya Afya namna ya kujikinga na maambukizi ya Corona.

Amewataka watanzania kuendelea kuzingatia mambo ambayo yanasaidia kupunguza Corona ikiwemo kufanya mazoezi, kunywa juisi ya Tangawizi na kujifukiza, amesema ugonjwa upo nchini hivyo ni muhimu Watanzania kujua umuhimu wa kujikinga.

Ameongeza kuwa mbali na kujifukiza tahadhari zingine za kuchukua kwa Watanzania ni kunawa mikono kwa maji tiririka na kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko ya watu, huku akisema wapo wagonjwa wachache wa Corona nchini hivyo Watanzania wawaombee, kwani jukumu la serikali ni kutoa huduma kwa wanaofikwa na ugonjwa huo.