Back to top

Watanzania washauriwa kuondoka Ukraine

24 February 2022
Share

Ubalozi wa Tanzania, Stockholm umetoa ushauri kwa Watanzania waishio Ukraine kuwa kama wanadhani kukaa kwao Ukraine siyo muhimu kwa sasa, waondoke nchini humo kutokana na kuwepo kwa hali tete ya kiusalama na kusasabisha mashaka juu ya usalama wao ambapo pia umewataka wazazi wenye watoto wanaosoma nchini humo kufanya taratibu binafsi za kuwarudisha watoto wao nyumbani kwa kutumia ndege binafsi zinazofanya safari kutokea Ukraine.