Back to top

Watanzania watakiwa kumuenzi Marehemu Sokoine kwa vitendo.

12 April 2018
Share

Rais Dokta. John Pombe Magufuli katika kumuenzi marehemu Edawrd Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza amewataka watanzania kumuenzi kiongozi huyo aliyefariki dunia kwa ajali ya gari mkoani Morogoro Aprili 12 mwaka 1984 kwa kujenga umoja kwa watanzania wote, kupiga vita rushwa pamoja na kuchapa kazi ili kumuenzi kiongozi huyo kwa vitendo.

Rais Dokta. Magufuli katika ukurasa wake wa twitter amesema watanzania wanapoazimisha kifo cha marehemu sokoine wanapaswa kuiga mfano wake kwani alikuwa msema kweli asiyeogopa, mpiga vita rushwa, ufisadi, unyonyaji mzalendo wa kweli, na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa.

"Marehem Sokoine hatasahaulika katika historia ya Tanzania, ni wito wangu kwa watanzania tumuige na kumuishi. Ni rai yangu pia tumuenzi kwa kujenga umoja wetu , kupiga vita rushwa na kuchapa kazi . Mungu aiweke roho ya marehemu Edward Moringe Sokoine mahala pema peponi."Ameandika Rais Magufuli.