Back to top

Watanzania watakiwa kutoa ushirikiano kwa Mhe. Rais Samia Suluhu.

04 April 2021
Share


Viongozi wa Dini ya Kikristo Mkoani Morogoro wamewataka waumini wa dini hiyo na Watanzania kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, hatua itakayo wezesha kusukuma kwa kasi ya maendeleo ya taifa.

Askofu Ole Mameo ameyasema hayo wakati wa ibada ya Pasaka, ambapo pamoja na mambo mengine amesema Rais Samia Suluhu Hassan amebeba maono ya Watanzania katika kulijenga taifa.

Kwa upande wake, Mhashamu Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Askofu Telesphori Mkude amewataka waumini kuendelea kuiamini Serikali na wametakiwa kuliombea taifa.