Back to top

WATATU WAUAWA NA POLISI MKOANI GEITA

15 June 2023
Share

Watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na Jeshi la Polisi, katika majibizano ya silaha katika eneo la Nyankumbu mkoani Geita, wakati wakijiandaa kuvamia moja ya maduka ya miamala ya fedha kwenye eneo hilo.
.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi, mkoani humo, ACP Safia Jongo, amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kuvamia zaidi ya maduka 20 ya miamala ya fedha na kupora zaidi mil. 50/= kwenye matukio matano katika maeneo mbalimbali.
.
Baada ya kuuawa watuhumiwa hao wamekutwa na bunduki aina ya Marker Four pamoja na mapanga wanayodaiwa kuyatumia kuvunja maduka na kujeruhi walinzi.