Back to top

"WATENDAJI WABORESHE VIVUKO KIGAMBONI"-CHONGOLO

22 April 2022
Share

Katibu Mkuu wa CCM, Bw.Daniel Chongolo amewataka watendaji wa Vivuko vya Kigamboni kuhakikisha wanaboresha utendaji kazi wa vivuko hivyo baada ya kuona changamoto ya vivuko hivyo pamoja na nauli za daraja kwa wakazi wa Kigamboni Dar es Salaam.
  
Chongolo amebainisha kwamba anatambua changamoto zinazo wakabili wa kazi wa Kigamboni haswa nauli za daraja na changamoto ya kivuko na ndio maana ametoa maagizo kwa watendaji wa Kivuko kuhakikisha vivuko vyote vitatu vinafanya kazi.

Akiwa kwenye ziara anayoendelea nayo ya kutembelea matawi ya CCM Dar es Salaam ambapo alitembelea matawi ya Wilaya ya Kigamboni ndipo akabaini changamoto hizo sambamba na kufahamu kwamba vivuko viwili tu ndivyo vinavyofanya kazi ya kuhudumia wananchi na kusababisha kero ndipo akatoa maagizo kwa watendaji.

Katika hatua nyingine Chongolo ametoa rai kwa viongozi wa CCM kuacha kutengeneza viongozi wanaotegemea kubebwa kwa kuwafichia fomu wanachama wengine kwani kufanya hivyo ni sawa kutengeneza bomu, amesema chama hicho hakipo tayari kukumbatia viongozi wa aina hiyo.