Back to top

Watoa huduma za afya toeni huduma bora kwa wateja wa Bima ya Afya.

28 November 2019
Share

Watoa huduma za afya nchini wametakiwa kutoa huduma bora kwa wateja wa Bima ya Afya kulingana na michango ya fedha zao wanazochangia ili wananchi waone umuhimu wa kulipia na kuwa na Bima ya afya.

Kauli hiyo imetolewa na Spika wa bunge Mstaafu na Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa taifa wa bima ya afya Mh Anne Makinda wakati wa uzinduzi rasmi wa vifurushi vya bima ya mfuko huo ambapo amesema wakati mwingine kinachowavunja moyo wananchi kujiunga na bima ni huduma hafifu wanazopata hivyo vyema watoa huduma wakajirekebisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa tiba wizara ya afya Dkt Grace Maghembe amesema mpango huo ni katika juhudi za serikali kuhakikisha kila mwananchi  anakuwa na bima ya afya kwani tatizo wanalokutana nalo kama watoa huduma ni wananchi kushindwa kulipia huduma .