Back to top

Watoto mapacha walioungana wafariki kutokana na changamoto ya upumuaji

23 January 2021
Share

Watoto Mapacha walioungana Dorcas na Dorine wamefariki dunia katika hospitali teule ya wilaya ya Iringa Tosamaganga.

Taarifa iliyotolewa na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dokta Ismail Banoba imeeleza kuwa mapacha hao wamefariki baada ya kupata changamoto ya upumuaji.

Januari 19, 2021 serikali wilayani Iringa iliwakabidhi watoto hao mapacha walioungana, Dorcas na Dorine kwa masista wa shirika la Theresia wa mtoto Yesu ili kuwalea watoto.

Ikumbukwe tu kuwa shirika hilo ndilo liliwalea mapacha wengine Maria na Consolatha ambao waliofariki mwaka 2018 wakiwa na umri wa miaka 21.