Mkoa wa Kigoma umezindua chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka14 ambapo watoto zaidi ya elfu 33 wanatarajia kupatiwa chanjo hiyo huku takwimu zikionesha asilimia 3.3 ya wanawake elfu sita waliofanyiwa uchunguzi mwaka 2017 wakigundulika kuwa na viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi na wengine 13 wakiwa tayari wamekwisha athirika na ugonjwa huo.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Kigoma Paul Chaote amesema tatizo la ugonjwa huo kwa mkoa wa Kigoma ni kubwa na kwamba mkoa umekuwa ukifanya jitihada kadhaa za kuhakikisha idadi ya wagonjwa inapungua kwa kufanya kampeni ya upimaji wa mara kwa mara kwa wananwake.
Akizindua chanjo hiyo kwa Niaba ya mkuu wa mkoa wa Kigoma,Mkuu wa wilaya ya Buhigwe,BrigediaJjenerali Marco Gaguti amewataka viongozi wa serikali kuwa mfano kwa kupeleka familia zao kupata chanjo hiyo.