Back to top

Watoto wa wili wa familia moja wafariki kwa kuangukiwa Geita.

26 January 2021
Share

Watoto wawili wa familia moja katika kitongoji cha Kasesa kata ya Kaseme mkoani Geita wamefariki dunia huku wengine 7 wakinusurika kifo baada ya kuangukiwa ukuta wa nyumba yao iliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

ITV ilifika eneo la tukio na kushuhudia mamia ya wananchi wa eneo hilo wakiitoa miili ya marehemu hao katika vifusi vya udongo.

Baba mzazi wa marehemu hao Bwana Malimi Kengele amesema watoto wake tisa Mwenyezi Mungu amewasaidia na kujiokoa walipofukiwa na kifusi cha ukuta wa nyumba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Bwana Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.