
Ikiwa ni siku ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha imezindua mabaraza ya watoto na kuyapa mbinu za kujikinga na vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikiwemo ubakaji, ulawiti na ukeketaji, pamoja na kutoa taarifa za matukio hayo ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wahusika.
