Back to top

WATOTO WATEKWA NA BOKO HARAM NIGERIA

11 March 2024
Share

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, amelaani mashambulio yanayozidi kuripotiwa Kaskazini mwa Nigeria, ambako watoto wadogo na wanawake wanashambuliwa na kutekwa na wapiganaji wa kikundi cha Boko Haram.

Kupitia mtandao wa kijamii wa X Bw.Mahamat, amewataka waliotekeleza uhalifu huo wawarejeshe watoto waliotekwa mara moja kwa familia zao.

Amesema kitendo hicho ni ishara kwamba tishio la ugaidi na wizi wa mifugo ni masuala yanayotishia sio tu usalama wa eneo hilo bali eneo zima na hata mataifa jirani na ni jambo ambalo linasikitisha wote barani Afrika.

Alhamisi iliyopita, wanafunzi takriban mia tatu walitekwa nyara na wapiganaji waliokuwa na silaha waliotumia pikipiki kuishambulia shule ya umma katika jimbo la Kaduna.