Back to top

Watoto wawili wachinjwa , miili yatupwa shambani.

16 June 2022
Share

Watoto wawili wenye umri wa miaka miwili na mwingine miaka saba, wakazi wa Kata ya Shabaka ,wilayani Nyangwale, mkoani Geita , wameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana, kisha miili yao kutupwa shambani, huku wauaji hao  wakitokomea pasipojulikana, hali iliyozua taharuki na hofu ya usalama wa watoto katika kata hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe anasema tayari wanamshikilia mganga wa kienyeji,mfanyabiashara na kikongwe mmoja kuhusu tukio la mauaji hayo.