Back to top

WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA MOTO KAGERA

04 July 2023
Share

Watoto wawili wa familia moja, waliojulikana kwa majina ya Mariam Mateso na Laurent Mateso, wote wakiwa na umri chini ya miaka 5, wakazi wa Kijiji cha Kanyamika, kilichopo wilayani Muleba, mkoani Kagera, wamefariki, baada ya nyumba waliokuwa wanaishi kuungua moto wakiwa ndani ya nyumba hiyo, ambapo baba wa watoto hao, Bw.Mateso Deus amesema kuwa tukio hilo la kuunguliwa nyumba ni la pili kwa familia hiyo, huku akiyahusisha matukio hayo na mtu anayeishi na mkewe kwa sasa.
.
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt.Aberl Nyamahanga, amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo, kutokana na familia kugubikwa na migogoro, iliyopelekea mama wa watoto hao kukimbia familia yake.