Back to top

Watoto zaidi ya milioni 3 wabainika kuwa na utapiamlo nchini.

02 August 2020
Share

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Mhe.Ummy Mwalimu amewataka wazazi nchini kuboresha lishe kwa watoto wao kufuatia utafiti uliofanywa kuonesha kuwa katika watoto milioni 9 wenye umri wa chini ya miaka 5, kati yao milini 3 wamebainika kuwa na utapiamlo.

Akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji nchini iliyofanyika kitaifa wilayani muheza, Waziri Ummy amesema katika mkoa wa Tanga takwimu zinaonesha kuwa umeathirika kwa asilimia 34% huku kitaifa ni asilimia 31% hatua ambayo imesababisha makundi hayo kusumbuliwa na udumavu uliopitiliza.
 
Katika maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yamefanyika katika viwanja vya jitegemee wilayani Muheza yenye kauli mbiu 'Tuwawezeshe wanawake kuwanyosha watoto kwa afya bora na ulinzi wa mazingira' Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajaat Mwanasha Tumbo amesema utafiti uliofanywa umeonesha kuwa wilaya yake ina watoto walemavu zaidi ya 800 kutokana na lishe duni.

Kufuatia hatua hiyo utafiti uliofanywa na wadau wa maadhimisho hayo umebaini kuwa asilimia 53% ya akina mama ndio wenye uwezo wa kunyonyesha mtoto saa moja baada ya kujifungua huku asilimia 56% ndio wanaoweza kunyosha ndani ya miezi 6.