Back to top

Watoto zaidi ya watano hupoteza maisha kila mwaka katika visima.

12 April 2019
Share

Ukosefu wa maji safi na salama katika kata ya Namiyonga wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma umekuwa ukisababisha watoto  wasiopungua watano kila mwaka kupoteza maisha katika visima vya kienyeji huku wanawake wakidai kutembea zaidi ya kilomita tano kutafuta maji.

Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kata ya Namiyonga yenye vijiji saba baadhi ya wanawake wameelezea madhila wanayokutana nayo kutokana na uwepo wa tatizo la maji likiwemo kutembea umbali mrefu, ambapo diwani wa kata hiyo Salima Limbalambala amesema ukosefu wa maji umeacha makovu makubwa katika eneo hilo.

Akizungumzia hilo Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homela amesema katika kuondoa kero hiyo baadhi ya wafadhili wameguswa na sasa wameanza uchimbaji wa visima.