Back to top

Watu 15 washikiliwa na Polisi kwa kosa la kukutwa na pembejeo feki.

31 July 2021
Share

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara  linawashikilia watu  kumi na tano kwa tuhuma za kukutwa na tani themanini na nne  nukta tatu  za  pembejeo ya unga  aina ya Salfa, pamoja na dawa ya maji  pisi miambili na tisini na mbili zikiwa zimeisha muda wake, ambapo kiwango kikubwa cha dawa hizo zinatumika kupambana na  magonjwa  yanayo sumbua mikorosho.

 

Dawa hizo zilikamatwa katika  wilaya ya Tandaimba na Mtwara.

 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bregedia General Marco Gaguti, amesema pembejeo hizo zimekamatwa katika  baadhi ya maduka yanayouza pembejeo.

 

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa  wa Mtwara Mark Njera amesema zoezi hilo limefanyika kwa muda wa siku mbili katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara .