Back to top

Watu 152 wanusurika kifo baada ya kula chakula cha sherehe Kigoma.

19 October 2020
Share

Watu 152 wakwemo watoto 79 wakazi wa kijiji cha Kigadye katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wamenusurika kufa baada ya kula chakula kinachodaiwa kuwa na sumu wakati wakishiriki sherehe ya kuzaliwa kwa watoto wa mkazi wa kijiji hicho aitwaye Tanu Zimbwe.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mikoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi James Manyama amesema Jeshi hilo kwa kushirikiana na timu ya afya kutoka halmashauri ya wilaya ya Kasulu ilifika eneo la tukio na kutoa huduma ya kwanza na baadae  kuwafikisha watu hao katika kituo cha afya cha Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na wengine kupelekwa hospitali ya wilaya ya Kasulu kwa matibabu zaidi.

Akizungumza kwa kwa njia ya simu na Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Daktari Robert Rwebangira amekiri kuwapokea watu thelathini na nne na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kasulu.