Back to top

Watu 157 wafariki baada ya ndege ya shirika la Ethiopia kuanguka

10 March 2019
Share

Shirika la Utangazaji la Serikali ya Ethiopia limetangaza kuwa watu wote waliokuwa kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines aina ya Boeing 737 – 800MAX iliyoanguka leo saa mbili asubuhi wamekufa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo yupo kwenye eneo la ajali na amethibitisha kwamba wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wamekufa.

Ndege hiyo inayodaiwa kununuliwa Novemba mwaka jana, ilikuwa inatoka Addis Ababa kwenda Nairobi, Kenya na ilianguka dakika sita tu baada ya kuruka.