Back to top

Watu 16 wakamatwa kwa makosa mbalimbali Tarime.

15 April 2018
Share

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara,limefanikiwa kuwakamata watu kumi na sita kwa tuhuma za kujihusisha na kilimo na biashara ya zao haramu la Bangi,mauaji na wizi wa mtoto.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya Kamishina Msaidizi wa jeshi la Polisi Henry Mwaibambe,amesema katika oparesheni hiyo Magunia  34 ya Bangi kavu yakiwa tayari kwa kuuzwa,Mirungi kilo 75,huku watu wawili wakikamatwa kwa tuhuma za mauaji na wizi wa mtoto mwenye umri wa miaka minane.

Kwa sababu hiyo kamanda huyo wa jeshi la polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya,amesema kuwa tangu tamko la rais kuhusu Polisi kutojihusisha na ufyekaji wa mashamba ya Bangi, bali kazi hiyo ifanywe na wananchi wa kijiji husika,tayari wananchi wameitikia wito kwa kuanza kutoa taarifa kuhusu watu wanajihusisha na kilimo cha zao la bangi.