Back to top

WATU 17 WAFARIKI KWENYE AJALI MKOANI TANGA

04 February 2023
Share

Watu 17 wamefariki duniani na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi dogo aina ya Costa iliyokuwa inasafirisha maiti na kugongana uso kwa uso na gari la mizigo aina ya Fuso katika eneo la Madira gerezani Korogwe mkoani Tanga.

Taarifa ya awali iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Bw.Omary Mgumba, aliyefika eneo la tukio la ajali imesema watu 17 walifariki eneo la tukio la wanaendelea kufuatilia hali za majeruhi na kutoa taarifa rasmi ya tukio la ajali hiyo ambayo imetokea majira ya saa tano na nusu usiku wa kuamkia leo.