
Watu 18 wamefariki dunia baada ya mlipuko kutokea katika kiwanda cha fataki katikati mwa mji wa Thailand
Polisi wameliambia shirika la habari la AFP kwamba serilali ya nchi hiyo inaendelea kufuatilia idadi rasmi ya vifo hivyo kwa sababu hawaoni uharibifu zaidi katika majumba mengine au watu wanaoishi karibu na jamii hiyo.
Picha zilizosambazwa na huduma ya uokozi wa eneo hilo zimeonyesha kifusi cha chuma kikiwaka moto ardhini, na moshi mweusi ukiwa umetanda, hata hivyo hakuna ishara yoyote inayoonyesha nini kimesababisha mlipuko huo.
