Back to top

Watu 2,160 wapoteza maisha kutokana na ajali za Bodaboda.

09 September 2019
Share

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Masauni amesema kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi Juni 2019 jumla ya  watu 2,160 wamepoteza maisha kutokana na ajali zilizotokana na bodaboda katika maeneo mbalimbali nchini.

Mhe.Masauni ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe.Emanuel Mwakasaka mbunge wa Tabora aliyetaka kujua zoezi la ukamataji waendesha pikipiki limekuwa na mafanikio kiasi gani.

Mhe.Masauni akasema kuwa vifo vilitokana na  ajali 5,213 zilizotokea kwa kipindi hicho na kuongeza kuwa mbali na idadi hiyo na ajali pia Jumla ya watu 4,209 walipata majeruhi.

Akaongeza kuwa chanzo kikubwa cha ajali za barabarani huchangiwa na waendesha pikipiki  kutofuata taratibu na kanuni za usalama barabarani.

Hata hivyo Mhe.Masauni amesema kila mwaka ajali zinazidi kupungua kutokana na usimamizi wa sheria ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuwakamata waendesha pikipiki wanaokiuka sheria na kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.