Watu 28 wafariki baada ya Lori la mafuta kupinduka na kuwaka Moto.

Watu ishirini na wanane wamefariki dunia baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto katika jimbo la Kogi, katikati mwa Nigeria.

Msemaji wa Idara ya Usalama wa Barabarani nchini humo Bisi Kazeem amesema watoto tisa ni miongoni mwa waliofariki dunia katika ajali hiyo iliyotokea karibu na kituo cha kuuzia mafuta katika barabara kuu ya Lokoja-Zariagi.

Gavana wa jimbo hilo, Yahaya Bello amesema ajali hiyo pia imeharibu idadi kubwa ya magari, majengo na vitu vingine vya thamani.

Mapema mwaka 2019 watu kadhaa walifariki dunia katika mlipuko wa lori la mafuta katika eneo la Odukpani katika jimbo la Cross River kusini mashariki mwa Nigeria.