Back to top

WATU 400 WAFARIKI KWA MAFURIKO AFRIKA KUSINI

17 April 2022
Share

Watu 400 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 20 hawajulikani walipo kufuatia mvua inayoendelea kunyesha Mashariki mwa Afrika Kusini na kuwaacha mamia kwa maelfu bila makazi.Vikosi vya uokozi vimewekwa katika hali ya juu ya tahadhari huku juhudi za kusambaza msaada wa kiutu zikiendelea katika jimbo la Kwa Zulu Natal kunakoshuhudiwa uharibifu mkubwa uliotokana na mafuriko.

Serikali imethibitisha kutokea kwa vifo kutokana na mvua kubwa ilipolipiga jimbo hilo na kusababisha pia uharibifu wa miundombinu usio na kifani katika historia ya Afrika Kusini.

Hadi sasa mafuriko hayo yameharibu nyumba 13,500, kiasi hospitali na kliniki 58 pamoja na mifumo mingine ya mawasiliano, usambazaji wa maji, nishati na barabara.