Back to top

Watu 48 wafariki kutokana na mafuriko Kenya.

07 November 2019
Share

Watu 48 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyobabishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini Kenya . 

Msemaji wa serikali Kanali mstaafu Cyrus Oguna amesema   zaidi ya mifugo elfu 17,550 imesombwa na maji huku watu zaidi ya  elfu 65 wakikosa makazi.

Serikali ya Kenya imesema  shirika la Red cross linafanya jitihada i za kusambaza chakula kwa waathirika wa mafuriko hayo na kwamba  raia atakayepoteza maisha kwa kukosa chakula.

Kuhusiana na Mitihani ya Taifa  ya shule za Upili ya kidato cha nne KCSE inayoendelea serikali imebainisha kuwa wanatumia helikopta kusambaza mitihani  katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.