
Watu 500 wanahofiwa kufariki dunia kwenye shambulizi ambalo limefanywa katika hospitali ya Ahli Arab, iliyopo Ukanda wa Gaza kutokana na shambulizi la angani, Wizara ya afya ya Hamas imedai Israel ndio imehusika.
Jeshi la Israel limekana kuhusika na kusema roketi ya wanamgambo wa Kiislamu huko Gaza ndiyo imepiga hospitali.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, ametangaza siku tatu za maombelezo baada ya mashambulizi hayo.
Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amelaani shambulizi hilo na kutaka ulinzi wa haraka kwa raia kwenye vituo vya afya katika eneo hilo la Palestina.
