Back to top

WATU 6 WAFARIKI 10 WAJERUHIWA MWANZA, DEREVA AKIMBIA

22 July 2023
Share

Watu 6 wote wakiwa wanaume wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa mara baada ya kugongwa na gari wakati wakifanya mazoezi ya kukimbia katika barabara ya Kiseke Manispaa ya Ilemela.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gidion Msuya, amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa dereva wa gari hiyo yenye namba za usajiri T476 DZL  Hilux Double Cabin ambaye hajatambuliwa mpaka sasa na amekimbia na kulitelekeza gari ambapo juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Miili ya marehemu imepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou-Toure, huku majeruhi 4 kati ya kumi hali zao zikiwa mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu.