Back to top

WATU 6 WAUAWA NA WENGINE 81 KUJERUHIWA HUKO INSTANBUL.

14 November 2022
Share

Takriban watu sita wameuawa na wengine 81 kujeruhiwa katika mlipuko katika eneo lenye shughuli nyingi katikati mwa Istanbul.

Gavana wa Jiji la Uturuki, Ali Yerlikaya amesema mlipuko huo umetokea kwenye barabara ya maduka katika eneo la Taksim Square, Mshukiwa sasa amekamatwa.

Makamu wa Rais Fuat Oktay, amesema mlipuko huo ulidhaniwa kuwa ni shambulio la kigaidi lililotekelezwa na mwanamke.

Rais Recep Tayyip Erdogan, amesema wahusika wataadhibiwa.