Back to top

Watu 8 wa 'familia moja'wakutwa wamekufa katika hifadhi ya Isawima.

10 September 2020
Share

Watu 8 wanaosadikiwa kuwa wa familia moja wakiwemo watoto watano wamekutwa wamekufa huku baadhi ya miili ya marehemu hao ikiwa imeteketea kwa moto katika hifadhi ya Isawima wilayani Kaliua mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi wa Polisi Barnabas Mwakalukwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo pamoja na watu wanaohusika kutekeleza unyama huo. 

Katika hatua nyingine kamanda mwakalukwa amesema jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kumvamia na kumpora mfanyabiashara mkazi wa tumbi manispaa ya Tabora huku pia likiedelea kuwaonya wale wote wanaoendelea kujihusisha na matukio ya kihalifu mkoani Tabora.