Back to top

Watu 80 watengwa na kupigwa marufuku kupata huduma na kijiji Rukwa.

14 February 2020
Share

Familia moja yenye kaya saba katika kijiji cha Katete wilayani Nkasi mkoani Rukwa wameiomba serikali kuingilia kati maamuzi ya wakazi wa kijiji hicho ambao wameamua kuwatenga na kuwapiga marufuku kupata huduma yoyote ya kijamii kijiji hapo kutokana na migogoro ya ardhi yao wanayoimiliki.

Familia hiyo ambayo  ina watu takribani themani inadai kuanza kukumbana na mkasa huo baada ya kushtaki mahakamani wakipinga maamuzi ya baraza la ardhi ya kata ambalo liliamuru kunyang’anywa kwa sehemu ya mashamba yao wanayodai walinunua kihalali kuanzia mwaka 2000.