Back to top

Watu milioni 7 kufikiwa na TASAF kipindi cha pili awamu ya tatu.

01 July 2020
Share

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umekusudia kuzifikia kaya maskini zaidi milioni 1.4 zenye walengwa zaidi ya watu milioni saba katika kipindi cha pili awamu ya tatu ya TASAF huku lengo kubwa ikiwa ni kuzifikia kaya zote zilizobakia Tanzania Bara pamoja na wilaya za Zanzibar kuziwezesha kaya maskini kukuza kipato na kuondokana na umaskini.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bi. Mercy Mandawa wakati akiongea na wawezeshaji watakaofanya kazi ya uhakiki wa kaya maskini katika Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma na kwamba mpango huo utafanyika katika halmashauri zote Tanzania Bara na wilaya za Zanzibar.