
Watu 8 wamejeruhiwa baada ya gari aina ya Noah yenye namba za usajili T 361 DMG, waliyokuwa wakisafiria kutoka mkoani Mbeya kuelekea mkoani Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori la mizigo aina Fuso, lenye namba za usajili T 632 CYP, katika eneo la hifadhi ya Taifa ya Mikumi, iliyopo mkoani Morogoro.
Akizungumzia tukio hilo, shuhuda wa ajali hiyo, ambaye ni Dereva wa Fuso, iliyohusika kwenye ajali hiyo, Edward chula amesema, chanzo cha ajali hiyo, ni dereva wa Noah kusinzia kisha kuligonga lori la mizigo lililokuwa mbele yake, kisha kupoteza uelekeo na kugongana uso kwa uso na Fuso.