
Watu saba wamefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori aina Scania, Trekta na Bajaji katika eneo la Mtaa wa Kidulya nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu ambapo katika ajali hiyo Bajaji iliwaka moto na kuteketea kabisa huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni mwendokasi wa dereva wa lori uliosababisha kugonga Bajaji.
