Back to top

Watu sita wafariki kwa ajali Monduli

20 April 2022
Share

Watu sita wamefariki dunia huku wengine wanne wakijeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T 189 DFY kugongana na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 250 CAA katika eneo la Alkatani Kata ya Sepeko wilayani Monduli ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akibainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori kushindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kuligonga gari aina ya Toyota Noah.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo akiwa eneo la tukio.


Hata Hivyo, Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa lori aliyesababisha ajali hiyo.