Back to top

Watu wanne wafariki wilayani Momba kwa kula nyama yenye kimeta.

09 January 2019
Share

Watu 4 wamefariki dunia katika kijiji cha Nzoka kata ya nzoka wilayani Momba mkoa wa Songwe baada kudaiwa kula nyama ya ng'ombe anayetajwa kufa  kwa ugonjwa wa kimeta ambapo hadi sasa zaidi ya watu wengine  74 wamebainika kupata dalili za ugonjwa wa huo wa kimeta.

Mkuu wa wilaya ya Momba Juma Said Irando amethibitisha kuwa matokeo ya vipimo vilivyofanyika, yameonyesha kwa asilimia 50 ugonjwa huo ni kimeta .