Back to top

Watu wanne wahukumiwa kunyongwa Songwe.

17 September 2019
Share

Mahakama kuu kanda ya Mbeya imewahukumu watu 4 kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuua kwa kusudia kinyume cha kifungu cha sheria namba 196 cha kanuni ya adhabu ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Akisoma hukumu hiyo leo 17 Septemba mkoani Songwe Jaji wa mahakama hiyo Dr. Adam Mambi amesema  mahakama imejiridhisha pasi na shaka kufuatia ushahidi uliotolewa na kujihoji kuhusu lengo la watuhumiwa.

Jaji Dr. Mambi amewataja washitakiwa hao kuwa ni Nathan Elias (31) mkazi wa Mwaka Tunduma, Moses Kasitu (26) mkazi wa Kilimahewa Tunduma na Elias Mzumbwe(23) mkazi wa Ihanda Mbozi, ambao wote walishiriki kumuua Vasco Njowela kwa  risasi  na kumnyang'anya mfuko uliokuwa na fedha za mauzo ya dukani sh. Million 1.