Back to top

Watu watano wafariki katika ajali ya gari – Kagera.

31 July 2021
Share

Watu watano wamefariki dunia baada ya basi la abiria la  kampuni ya Frester kugongana na gari dogo aina Corora katika eneo la Kasindaga wilayani Biharamuro mkoani Kagera, wakati gari hiyo ndogo ilikuwa ikitokea wilaya ya Muleba kuelekea mkoani Geita.

Mganga Mkuu wa Hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo Dr. Gresmus Sebuyoya amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo miili ya marahemu imehifadhiwa katika hospitali hiyo.

ITV ilimtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi Revocutus Malimi na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu wa tano.