Back to top

Watu wawili mbaroni kwa kuhusika na wizi wa bajaji Morogoro.

12 February 2019
Share

Watu wawili Mwanamke na Mwanaume ambao majina yao yamehifadhiwa wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuhusika na mtandao wa wizi wa bajaji ambao wanatumia mbinu ya kuwatumia wanawake kama chambo wakijifanya abiria badae wanawapulizia madawa ya kulevya madereva hao na kuwaibia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amethibitisha tukio hilo ambapo amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa maeneo ya Rungemba Manispaa ya Morogoro ambapo mtuhumiwa wa kike alijifanya abiria kukodi bajaji ya Omary Ally kwenda katika nyumba ya wegeni Kisha kumpa kinywaji ambacho kinadaiwa kuwa na madawa ya kulevya aina ya ugoro.