Back to top

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni mtu na mkewe wanusurika kufa.

16 June 2018
Share

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni mtu na mkewe  wamenusurika kufa katika ajali baada ya gari ndogo  aina ya Noah waliyokuwa wakisafiria kugongana na gari jingine aina ya Ford na kupinduka katika eneo la Kidatu mkoani Morogoro,  katikati ya mpaka wa daraja linalounganisha wilaya za kilombero na kilosa.

Ajali hiyo imehusisha gari aina Noah yenye namba za usajili T 491 DES iliyokua ikitokea Morogoro kuelekea kKilombero iliyoigonga gari nyingine aina ya Ford yenye namba T 757 DHF   na kugonga daraja na kupinduka ambapo mashuhuda wamedai dereva wa noah alikuwa akijaribu kukwepa korongo  lililo karibu na daraja.

Dereva wa Noah alikataa kuzungumza lolote kuhusiana na ajali hiyo ambapo wasamaria wema walifanya jitihada za kuwaokoa watu hao na kupisha shughuli za usafiri zilizokwama kwa muda kuendelea, huku mwenyekiti wa kitongoji cha Mang'ula kidatu akawasihi madereva kuwa makini barabarani.