Back to top

Watu wawili wanatafuta kufuatia tukio la ng’ombe vibudu Tegeta.

13 May 2018
Share

Hali ya sintofahamu imezuka  eneo la Tegeta machinjioni baada ya mizoga ya ng'ombe 15  kupelekwa katika machinjio hayo kwa  ajili ya kuchinjwa na baadhi ya mizoga hiyo ya  ng'ombe  kuchinjwa tayari kwa ajili ya kusambazwa katika mabucha ya kuuzia nyama jijini Dare s salaam.

ITV  ilifika katika eneo hilo la Tegeta machinjioni na kukuta gari aina ya Isuzu lenye namba za usajili T 486 DHZ lililokuwa na mizoga hiyo ya ng'ombe likiwa limetelekezwa hali iliyolazimu ng'ombe hao kupakiwa katika gari jingine ili wapelekwe kuharibiwa.

Katika eneo hilo maaskari kutoka mkoa wa  Kipolisi wa Kinondoni walilazimika kuimarisha ulinzi ili  kuzuia uwezekano wa baadhi ya watu kujichukulia nyama kutoka katika mizoga hiyo na kwenda kuitumia ama kuiuza.

ITV ilifanya jitihada za kuzungumza na Maafisa wa serikali walikuwepo eneo la tukio ambao walikataa kuzungumza na  hivyo kumtafuta Meya  wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta ambaye alizungumza kwa njia ya simu na kukiri kutokea tukio hili na kuwa watu wawili waliokuwa na mizoga hiyo ya ng'ombe wanatafutwa kwani walikimbia baada ya tukio kubainika.