Back to top

Watu wawili wauawa kwa tuhuma za wizi wa kuku Mwanza.

16 April 2021
Share

Kwa mara nyingine tena kata ya Kishiri iliyopo wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, ambayo wiki mbili zilizopita ilikumbwa na taswira hasi ya mauaji ya kijana George Kusekwa kwa tuhuma za kuiba ndala, Usiku wa kuamkia leo tena wananchi wa mtaa wa Bukaga kata ya Kishiri wamejichukulia sheria mkononi na kuwaua watu wawili ambao majina yao hayajafahamika kwa kuwapiga mawe na baadaye miili yao kuchomwa moto na wananchi wa mtaa huo.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Ssalama wilayani humo Dk.Philis Nyimbi, amempa saa 12 mkuu wa polisi wa wilaya hiyo kuwakamata watuhumiwa wote waliohusika na mauaji hayo na kuwakemea vikali watu wanaojichukulia sheria mkononi.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Philis Nyimbi.