Back to top

WATU ZAIDI YA 24 WAMEUAWA NA TEMBO TUNDURU

26 May 2023
Share

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas amesema katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia Mei, 2023, zaidi ya watu 24 wameuwawa kwa kukanyagwa na wanyama aina ya tembo huku wengine 21 wakijeruhiwa katika Wilaya ya Tunduru mkoani humo ambapo ameshukuru jitihada za serikali na wadau mbalimbali kwa kuendelea kuchukua hatua za kukabiliana na wanyama hao.
.
Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo, baada ya kukabidhiwa kwa magari 4, pamoja na pikipiki 16 zenye thamani ya zaidi ya Tshs.Mil. 350/=, yaliyotolewa na serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani kwa ajili ya Wilaya za Namtumbo na Tunduru mkoani humo.