Back to top

WATU ZAIDI YA 50 WAFARIKI KUTOKANA NA NJAA TIGRAY

24 November 2023
Share

Zaidi ya watu 50 wamefariki dunia kutokana na njaa iliyosababishwa na ukame katika majimbo ya Tigray na Amhara Kaskazini mwa Ethiopia.

Ofisi ya Kudhibiti Hatari ya Majanga Tigray imesema watu arobaini na waliokimbia makazi yao wamekufa baada ya kuwa tayari wameacha makazi yao kwa sababu ya ukame.

Mkuu wa ofisi hiyo Gebregziabher Gebrehiwot amesema katika eneo jirani la Amhara la Wag Hemra, takribani watu sita na ng'ombe elfu nne  wamekufa kwa sababu ya uhaba wa chakula uliosababishwa na ukame.