
Jeshi la Polisi Nchini Kupitia Kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya (Anti Drug Unit) 'ADU' limesema katika kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba, 2022, jumla ya kesi 369 zilifikishwa mahakamani na kutolewa maamuzi, ambapo watuhumiwa 377 walitiwa hatiani, 170 wamefungwa vifungo mbalimbali na 207 wamelipa faini na kuachiwa huru, huku vyombo vya moto (Magari 8, Pikipiki 9, Boti 02) na Nyumba 01 vikitaifishwa na Mahakama, na kuwa Mali za Serikali.