Back to top

Watuhumiwa 15 mbaroni kwa mauaji Tunduru-Ruvuma

24 September 2022
Share

Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo nchini, linawashikilia watuhumiwa 15 waliohusika katika tukio la mauaji ya wafugaji katika kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji nchini, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Pasua ameeleza hayo alipofika Kijiji cha Mbatamila wilaya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa kumi na tano (15) kwa kosa la mauaji ya vijana wanne wa familia moja katika Kijiji cha mbatamila nakusema kuwa wale wote waliofanya mauaji hayo hawako salama nakuwataka wajisalimishe Jeshi la Polisi.

Aidha amewataka wakulima na wafugaji kutojichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate misingi ya sheria na taratibu katika kutatua Changamoto zilizopo.

Sambamba na hilo amewapa pole wananchi waliopoteza ndugu zao ambapo kamanda Pasua amesema Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wote walio baki ili wafikiahwe katika vyombo sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.