Back to top

WATUHUMIWA 4 UKATAJI MAPANGA MBARONI, SHINYANGA

26 July 2023
Share

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, limefanikiwa kukamata bunduki 5 na risasi zaidi ya 300 zilizokuwa zimefichwa kwa kufukiwa ardhini na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu, pamoja na vifaa vya kupigia Ramli Chonganishi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Leonard Nyandahu, ambapo ameeleza kuwa wamekamata watuhumiwa 4 ambao wamekuwa wakikodiwa na kujihusisha na mauaji kwa kuwakata watu mapanga.

Amesema kwa kipindi hicho wamekamata vitu mbalimbali vya wizi yakiwamo Matairi 5, Mafuta ya dizeli lita 310, yaliyoibwa katika Mradi wa SGR, Waya wa Fensi Mita 12 mali idhaniwayo ya Mgodi wa Buzwagi, na vifaa vya kupigia Ramli Chonganishi.

Aidha, amesema pia wamekamata Bunduki 5 na Risasi zaidi ya 300, ambazo zilikuwa zimekodishwa katika makampuni ya ulinzi na watu binafsi kinyume na taratibu.

"Katika Msako huu licha ya kukamata vitu mbalimbali vya wizi, pia tumekamata watuhumiwa 4 ambao wamekuwa wakikodiwa kujihusisha na ukataji wa mapanga, na tumewahoji wamekiri kujihusisha na vitendo hivi katika maeneo mbalimbali"amesema Nyandahu.