
Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya, limesema limekamata tani 13.717 za dawa za kulevya Pamoja na watuhumiwa 4987 katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, ACP. Amon Kakwale amesema katika kipindi cha
kuanzia Januari hadi Juni 2023, walifanikiwa kukamata kiasi cha kilogramu 9,358.77 sawa na Tani 9.36 za dawa za kulevya aina ya bhangi, tani 4.357 za mirungi, kilogramu 1.86 za heroin pamoja na gramu 220.05 za cocaine, huku ekari 105.25 za mashamba ya bhangi na
mirungi zikiteketezwa.

