Back to top

Watuhumiwa 56 wakamatwa kwa kujihusisha na makosa ya wizi wa magari.

20 April 2021
Share

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mkuu wa Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Kamanda Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 56 wanaojihusisha na makosa ya wizi wa magari na pikipiki. 

Kamanda Mambosasa Amesema kuwa, Katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi Aprili, 2021 Jeshi la polisi limefanya operesheni mbalimbali ya kupambana na waharifu vinara wanaojihusisha na wizi wa magari pamoja na pikipiki katika jiji la Dar es salaam.

Aidha, Kamanda Mambosasa amesema kuwa Jeshi linaendelea na uchunguzi na watuhumiwa wanaendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi.