Back to top

WATUMISHI 7 KUCHUKULIWA HATUA, LIWALE

18 September 2023
Share

Waziri wa TAMISEMI, Mhe.Mohamed Mchengerwa ameagiza watumishi 7 wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi  kuchukuliwa hatua, kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, hali ambayo imedaiwa kuzorotesha utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za Halmashauri hiyo.
.
Mchengerwa ameyasema uamuzi huo wakati wa ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo.
.
Aidha, Waziri huyo amesema kuwa, kuanzia sasa Maafisa wote wenye kesi za rushwa na ubadhirifu wasihamishwe vituo kwenye vituo vyao vya kazi mpaka mashauri yao yanapokamilika.